Kuanzia Jumatano 31 Machi, wafanyakazi wa hospitali ambao hawaja chanjwa, hawataweza watibu wagonjwa wenye COVID-19 chini ya itifaki mpya.
Waziri Mkuu Scott Morrison na Gavana Mkuu David Hurley mapema hii leo walishiriki katika hafla yakuapisha baraza jipya la mawaziri wa shirikisho katika nyumba ya serikali. Ujumbe mpya wa baraza lamawaziri ume anzishwa, linalo lenga usawa wa wanawake, usalama, usalama wakiuchumi pamoja na afya.
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuharakisha kesi, kuondoa kesi zisizo na msingi na za kubambikizwa ili kuondokana na idadi kubwa ya kesi ambazo Serikali inashindwa. Rais Samia ameyasema hayo Jumapili, baada ya kupokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Takukuru Ikulu ya Chamwino, Dodoma.