Sheria mpya inayowasilishwa katika bunge la jimbo ya Victoria, itazipa shule mamlaka yakuzuia wazazi ambao hufanya vurugu kuingia katika viwanja vya shule. Sheria hiyo itawaruhusu walimu wakuu wa shule, kutoa amri za usalama wa jamii, kwa wazazi hao ila, kama mzazi hatii amri hiyo, swala hilo linaweza fikishwa mahakamani.
Rais wa Marekani Joe Biden, ambaye hapo awali aliamua kuacha idadi ya wakimbizi iliyowekwa na mtangulizi wake ambayo ilikuwa ni chini sana kihistoria ya kuruhusu wakimbizi wanaoingia kila mwaka, Jumatatu alitangaza kwamba anaongeza mara nne ya idadi hiyo mwaka huu. “Ninarekebisha kiwango cha juu cha idadi ya kukubaliwa kwa wakimbizi kuingia ya kila mwaka ya Marekani hadi 62,500 kwa mwaka huu wa fedha," rais Biden alisema katika taarifa Jumatatu alasiri.
Hali ya wasiwasi imeendelea kuongezeka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kufuatia mashambulizi mabaya ya Jumamosi, ambapo, wapiganaji waliwaua watu wasiopungua 19, wakiwemo wanajeshi 10, katika uvamizi wa vijiji viwili. Mashambulizi hayo yalifanyika saa chache baada ya Rais Felix Tshisekedi kutangaza hali ya tahadhari na kuzingirwa kwa majimbo mawili, na maafisa wa usalama.