Taarifa ya Habari 4 Septemba 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Mpango wa chama cha Labor kuzuia waajiri, kufuta makubaliano ya ajira yakasirisha upinzani wa shirikisho.


Upinzani wa shirikisho unaishtumu serikali kwakujaribu kushawishi mwamuzi huru wa ajira, baada yaserikali kutoa onyo kwa mipango yakujaribu kupunguza mamlaka ya waajiri kufuta mikataba ya kazi. Hata hivyo, waziri Brendan O'Connor ametupilia mbali madai ya upinzani.

Mashauriano juu ya mamlaka ya mikataba na kanuni za mapambano zinachelewesha kupelekwa kwa wanajeshi huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo chini ya jeshi la dharura la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Gazeti la The East Africa linafahamu kuwa nchi tano kati ya sita wanachama wa EAC – ikiwemo Kenya, Tanzania, Uganda na Sudan Kusini – ziko tayari kupeleka majeshi huko mashariki mwa DRC lakini zimesisitiza kuwepo kwa kanuni sahihi ili kuepuka makosa yaliyotokea katika vikosi vya awali vya kulinda amani.

Wakenya ndani na nje ya nchi waendelea kusubiri kujua kama uchaguzi wa urais utarudiwa au ushindi wa Dr William Ruto utaidhinishwa. Baada ya wiki nzima ya kila upande kutoa maombi na mawasilisho mbele ya majaji saba wa mahakama ya upeo, ngoja ngoja ya siku 14 sasa itafika tamati kesho ,Jumatatu tarehe 5.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa ya Habari 4 Septemba 2022 | SBS Swahili