Uamuzi wa Rais Donald Trump kuwaondoa wanajeshi wa Marekani nchini Somalia katika siku za mwisho za urais wake, umechochea malalamiko kutoka kwa baadhi ya Wasomali, ambao wamemuomba rais ajaye Joe Biden kubadili uamuzi huo.
Vita vya takribani mwezi mmoja vya Ethiopia katika jimbo la kaskazini la Tigray, vimeathiri kwa kiwango kikubwa jitihada za kukabiliana na janga la corona katika taifa hilo miongoni mwa yenye kiwango kikubwa cha maambukizi barani Afrika.
Chama cha upinzani cha ACT Wazalendo kimeafikia uamuzi wa kujiunga na serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa mujibu wa Ado Shaib katibu mkuu wa chama hicho. Katika mkutano maalum wa kamati kuu ya chama cha ACT Wazalendo, wameamua kuwa wapendekeze jina la mwanachama atakayekuwa makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar.