Rais mpya wa Marekani ameweka dhahiri kuwa ulimwengu utarajie Marekani yenye diplomasia zaidi kuelekea mbele akianza kwa kusitisha mpango wa rais aliyeondoka Donald Trump wa kuondoa maelfu ya wanajeshi wa Marekani walioko Ujerumani.
Kamanda wa zamani wa waasi wa Uganda Dominic Ongwen alikutwa na hatia Alhamisi kwa uhalifu wa vita na uhalifu mwingine dhidi ya ubinadamu. Tuhuma hizo ni pamoja na mauaji, manyanyaso ya kingono, kuwateka watoto, wizi wa ngawira, katika uamuzi kwenye mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa.
Rais wa Afrika Kusini ambaye pia ni mwenyekiti anayemaliza muda wake wa Umoja wa Afrika Cyril Ramaphosa amesema leo kuwa upatikanaji wa mikopo yenye masharti nafuu itakuwa jambo muhimu kuelekea ufufuaji wa uchumi wa mataifa ya Afrika ulioathiriwa na janga la COVID-19.