Kundi la wanawake pekee linalo simamia maswala ya usalama majina, lenye lengo lakuzisaidia jamii zawahamiaji kujiamini ndani ya maji, limerejea baada ya COVID-19 kuzuia mazoezi yao mwaka jana. Kundi hilo kwa jina la Swim Sisters, linalo jumuisha wanawake kutoka dini mbali mbali, linatumai kuwawezesha wanawake, kupata ujuzi wakuogelea baharini.
Tanzania imetoa onyo kali kwa wale wanaotoa na kusambaza taarifa za magonjwa ya mlipuko ikiwemo janga la Corona. Onyo hilo linatolewa wakati madhehebu ya dini yakieleza hali ilivyo katika taasisi zao kuhusiana na janga hilo ambalo linaendelea kuisumbua dunia. Msemaji Mkuu wa serikali Hassan Abbas amesema ni kinyume cha taratibu mtu kutoa taarifa zinazohusiana na majanga kama vile mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona.
Kenya imepiga marufuku mara moja ununuzi wa mahindi kutoka mataifa jirani ya Tanzania na Uganda. Kulingana na barua ilioandikwa na Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya kilimo na chakula, Kello Harsama kwa Pamela Ahago ambaye ni Kamishna wa forodha katika mamlaka ya ushuru nchini Kenya KRA, ununuzi huo umesitishwa baada ya uchunguzi kubaini kwamba mahindi kutoka mataifa hayo mawili sio salama kwa matumizi ya chakula cha binadamu. Mamlaka hiyo imekuwa ikifanya uchunguzi kuhusu usalama wa chakula kinachoingizwa nchini Kenya .