Chama tawala cha mseto kimeadhimisha siku yakina mama, kwa kutoa ahadi ya uchaguzi inayo lenga wazazi watarajiwa ambao wana magonjwa sugu saratani ikijumuishwa. Naye Kiongozi wa upinzani Anthony Albanese amehamisha mwelekeo wake wa kampeni ya uchaguzi, kwa kulenga haki ya malipo ya wanawake, katika hatua inayo fuata ya sera kwa ajili yakuwavutia wapiga kura.
Viongozi wa jamii zawa Afrika nchini Australia, wahamasisha chama kitakacho unda serikali mpya, kishughulikie malalamishi ya baadhi ya wanachama wa jamii yawa Afrika wanao dai wanabaguliwa kazini, wengi wao wakinyimwa kazi licha yakuwa na vyetu na uzoefu wakutosha kutekeleza majukumu ya ajira husika.
Benki kuu ya Uganda inatafakari kutoa sarafu ya kidigitali, na haijapiga marufuku sarafu ya kimtandao “cryptocurrencies” lakini ina wasiwasi kuhusu madhara ya kiteknolojia ikiwemo kumlinda mteja, na uhalifu wa kifedha amesema afisa mwandamizi wa benki kuu ya Uganda, Ijumaa.