Baraza la seneti la Marekani leo litaanza mchakato wa kusikiliza kesi inayomkabili rais wa zamani Donald Trump, wakati timu ya mawakili wa kiongozi huyo ikidai kwamba mashitaka dhidi yake ni kinyume na katiba.
Muungano wa vyama vya upinzani nchini Somalia umependekeza kuundwa kwa Baraza la Taifa la wabunge, viongozi wa upinzani na mashirika ya kiraia kuongoza taifa hilo la Pembe ya Afrika, baada ya muda wa rais kumalizika jana bila kuwepo na mpango wa kukabidhi madaraka.
Afrika Kusini imesitisha kwa muda kampeni yake ya chanjo dhidi ya COVID-19 Jumapili baada ya utafiti mpya kubaini kuwa chanjo ya AstraZeneca haifanyi kazi vizuri dhidi ya aina mpya ya virusi vinavyopatikana nchini humo. Shirika la Afya Duniani - WHO linafanya mkutano Jumatatu kuhusu maendeleo ya hivi karibuni nchini Afrika Kusini.