Katika taarifa zingine waziri mkuu Scott Morrison, kwa mara nyingine ametupilia wazo lakuanzisha uchunguzi huru kwa madai ya ubakaji dhidi ya mwanasheria mkuu Christian Porter. Bw Morrison amesema madai hayo yanastahili shughulikiwa kupitia mahakama na polisi, nasi kwa kile anacho ita chunguzi za ziada zakimahakama zinazo undwa na wanasiasa.
Meghan Merkel mke wa Prince Harry ameilaumu familia ya kifalme ya Uingereza kwa kuzua wasi wasi kutokana na rangi ya mwanaye swali llilompelekea kutafakari kuhusu kujitoa uhai. Hayo ameyasema wakati wa mahojiano Jumapili, swala ambalo huenda likazua hali ya taharuki kwenye familia ya kifalme ya Uingereza.
Serikali ya Kenya imesisitiza kuwa maisha ya raia wake ni muhimu mno kuliko kitu kingine, kufuatia hatua yake ya mwishoni mwa wiki kupiga marufuku mara moja ununuzi wa mahindi kutoka mataifa jirani ya Tanzania na Uganda kwa kile inakichokitaja ni kuwepo kwa viwango vya juu vya sumu kwenye mahindi hayo. Mamlaka ya kilimo na chakula nchini humo, ikijibu madai ya serikali ya Tanzania kuwa haijapokea ithibati rasmi ya marufuku hiyo, imeeleza kuwa malori yaliopo katika mpaka wa Namanga hayata ruhusiwa kuingia Kenya hadi suala hilo lisuluhishwe, kama anavyoripoti mwandishi wetu wa Nairobi, Kennedy Wandera.