Serikali imetangaza uwekezaji wa angalau dola bilioni 10 kwa huduma ya uzeeni ila, wanaharakati wanawasiwasi kuwa kupitia kupungua kwa uhamiaji, sekta hiyo haitakuwa na wafanyakazi wakutosha.
Mshukiwa wakuunga mkono kundi la wanamgambo wa daesh amerejeshwa Australia, baada yakuishi kwa miaka kadhaa nchini Syria na Uturuki. Mohamed Zuhbi mwenye umri wa miaka 30, alifikishwa mahakamani kupitia mitambo ya video mapema hii leo, kabla akabiliane na mashtaka kadhaa yakitaifa, yanayo jumuisha kuwasajili wapiganaji wakigeni kujiunga na shirika hilo lakigaidi.
Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa, ICC Alhamisi imemhukumu Dominic Ongwen, raia wa Uganda, ambaye zamani alikuwa kamanda wa kundi maarufu la waasi la Lord Resistance Army (LRA), kifungo cha miaka 25 jela, kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu. Dominic Ongwen, mwenye umri wa miaka 45, alipatikana na hatia mwezi Februari 2021, kwa mashtaka 61, yakiwa ni pamoja na mauaji, ubakaji na utumwa wa kijinsia, mwanzoni mwa miaka ya 2000, chini ya LRA, wakati huo likiongozwa na Joseph Kony, ambaye alitoweka, na hajulikani aliko.