Taarifa ya Habari 9 Mei 2025

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Anthony Albanese akosolewa kwa kumshasha cheo waziri pekee Muislamu katika baraza lake la mawaziri, wakati vyama vya upinzani vya ongeza juhudi yaku wachagua viongozi wao wapya.


Bunge la Ulaya limeidhinisha Alhamisi maazimio ya haki za binadamu kuhusu Tanzania, na kulaani hatua ya kutiwa nguvuni mwanasiasa Tundu Lissu ambaye ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo Chadema. Katika azimio lao, wabunge wa Ulaya wamelaani kukamatwa kwa kiongozi huyo na kueleza wasiwasi wao mkubwa kuhusiana na tuhuma za kisiasa dhidi yake ambazo hukumu yake huenda ikawa ni kifo.

Kardinali Robert Prevost ametangazwa kuwa kiongozi ajaye wa Kanisa Katoliki. Yeye ndiye Papa wa kwanza kutoka Marekani na kuchukua jina la papa Leo XIV. Kanisa Katoliki limempata Kiongozi wake mpya, Papa Leo wa 14 atakayewaongoza takriban waumini bilioni 1.4 kote ulimwenguni. Kiongozi huyo amepatikana Alhamisi jioni baada ya uchaguzi uliofanywa na makadinali wapatao 133 kutoka mataifa 70.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service