Hospitali za New South Wales zitapata nafasi zaidi za matibabu za muda mfupi ili kupunguza shinikizo kwa idara za dharura.
Sikiliza makala yetu yaliyo rekodiwa hapa
Serikali ya jimbo inawekeza zaidi ya dola milioni 130 katika vitengo kwa wagonjwa wanaotarajiwa kurudi nyumbani, au kuhamia katika kituo kingine cha utunzaji ndani ya saa 24.
Kiongozi wa jimbo la Magharibi Australia Roger Cook amekaribisha ahadi ya Waziri Mkuu ya kudumisha makubaliano ya GST ya jimbo hilo. Bw. Cook amekuwa akifanya kampeni dhidi ya pendekezo la Tume ya Uzalishaji ambalo linaweza kuigharimu Australia Magharibi mabilioni ya dola kwa mwaka.
Ujumbe wa kwanza wa aina yake umetumwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kufuatilia utekelezaji wa usitishaji mapigano kati ya jeshi la serikali na kundi la waasi la M23, linaloungwa mkono na Rwanda.Ujumbe huo umewasili mjini Minembwe, jimboni Kivu Kusini, eneo ambalo limekumbwa na mapigano makali katika miezi ya karibuni.
Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.






