Kiongozi wa jimbo la Victoria, Jacinta Allan, anasema hatajiuzulu kutoka wadhifa wake, miezi minne kabla ya uchaguzi wa jimbo hilo.
Wabunge wa chama cha Labor walikutana Jumapili usiku kujadili matarajio ya chama cha Labor katika uchaguzi huo na vyanzo vya habari katika mkutano huo vimeambia gazeti la The Age kwamba Bi Allan hana uungwaji mkono wa wengi wa wajumbe wa chama hicho. Licha ya shinikizo linalo mkabili, Bi Allan amewaambia wafuasi wake kwamba hana mpango wa kujiuzulu kama kiongozi.
Kinyang'anyiro cha kumpata kiongozi mpya wa Umoja wa Mataifa siku ya Jumamosi kimeongeza mgombea wa saba: Olara Otunnu wa Uganda, mgombea wa zamani wa urais na afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa. Otunnu alihudumu kama msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na mwakilishi maalum wa masuala ya watoto na migogoro ya silaha kuanzia 1997 hadi 2005 chini ya mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati huo Kofi Annan. Pia alihudumu kama mjumbe wa Umoja wa Mataifa wa Uganda, na kama waziri wa mambo ya nje wa nchi yake kwa muda mfupi.
Bofya hapo juu kwa taarifa zaidi.






