Usiku wa sensa ukikaribia, maafisa wa Ofisi ya Takwimu ya Australia wanawahimiza watu wanao ishi katika makaazi yenye watu wengi sana, wasiwe na hofu yakushiriki kwa sababu hapatakuwa athari yoyote ya kisheria.
Rais wa Klabu ya Soka na Netiboli ya Fitzroy ameambia uchunguzi wa shirikisho kuhusu ubaguzi wa rangi dhidi yawa Aboriginal na Wakaazi wa Visiwa vya Torres Strait, kwamba amepitia na kushuhudia kiwango kikubwa cha ubaguzi wa rangi. Anasema ubaguzi wa rangi unaathiri watu wa Mataifa ya Kwanza kote nchini, na lazima ushughulikiwe na ngazi zote za serikali.
Mkuu wa Shirikisho la Afya Duniani, WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus amefanya ziara nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kutahadharisha kwamba ugonjwa wa Ebola mashariki mwa taifa hilo unasambaa haraka mno. Akiwa nchini DRC, Ghebreyesus amesema anakutana na washirika wa afya na kiutu wanaosaidia mapambano dhidi ya Ebola nchini DRC kujadiliana changamoto zinazowakabili na kubainisha kuwa visa vipya "viliongezeka maradufu katika baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi wiki iliyopita.
Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.






