SKIP TO MAIN CONTENT

Taarifa ya Habari:Ripoti mpya yaitaka Australia iboreshe usalama wa dawa na itoe wakalimani kwa jamii za tamaduni mbalimbali

cabra pharmacy.jpg
Cabramatta East Day Night (Facebook)

Ripoti mpya imeangazia changamoto kubwa za usalama wa dawa zinazowakabili Waaustralia wenye tamaduni mbalimbali, na inatoa wito wa upatikanaji mkubwa wa taarifa na wakalimani wa dawa zinazotumia lugha nyingi.


Published

By Gode Migerano

Presented by Gode Migerano

Source: SBS


Skip to podcast episode content

Ripoti mpya imeangazia changamoto kubwa za usalama wa dawa zinazowakabili Waaustralia wenye tamaduni mbalimbali, na inatoa wito wa upatikanaji mkubwa wa taarifa na wakalimani wa dawa zinazotumia lugha nyingi.


Waziri Mkuu Anthony Albanese anasema atawasilisha hoja ya vurugu za kifamilia na za nyumbani, katika mkutano wa baraza la mawaziri la kitaifa wiki ijayo huku kukiwa na maswali kuhusu mipango ya kushughulikia mgogoro huo.

Watu saba, wakiwemo raia watano wa Marekani pamoja na mkuu wa ujasusi wa Ecuador, wamefariki baada ya helikopta ya kitalii waliyokuwa wakisafiria kuanguka katika kaunti ya Samburu, kaskazini mwa Kenya. Kwa mujibu wa ripoti ya awali kutoka Kituo cha Polisi cha Archers Post iliyoonekana na shirika la habari la Reuters, helikopta hiyo ilikuwa ikielekea katika Hifadhi ya Loisaba, eneo maarufu la uhifadhi wa wanyamapori na kivutio cha utalii kaskazini mwa Kenya, ilipoanguka.

Nchini DRC, upande wa mashtaka umeomba kifungo cha miaka 15 cha kazi ya kulazimishwa kwa Waziri wa zamani wa Sheria Constant Mutamba na Chancard Bolukola, mratibu wa zamani wa FRIVAO, Mfuko wa fidia kwa waathiriwa wa shughuli haramu wa Uganda. Kesi hiyo inahusisha dola milioni 65 ambazo Uganda imekuwa ikilipa kila mwaka kwa miaka mitano iliyopita, kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki.

Bofya hapo juu kwa taarifa zaidi.


Latest podcast episodes

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Stream now