Ada ya maombi ya visa ya mwanafunzi imeongezeka tangu Julai 1 kutoka $2,000 hadi $2,500, huku Visa ya Muda ya Uzamili, au visa nambari 485, sasa inagharimu $5,750.
Sikiliza makala yetu yaliyo rekodiwa hapa
Australia tayari ina moja ya ada za juu zaidi za maombi ya visa ya mwanafunzi duniani, na ongezeko la hivi karibuni limesababisha ukosoaji kutoka kwa baadhi ya wanafunzi wa kimataifa na mawakala wa uhamiaji.
Waziri wa Sekta ya Ulinzi Pat Conroy anasema sera ya ulinzi ya serikali, ikiwa ni pamoja na mradi wa AUKUS, ni mfano wa 'uzalendo unaoendelea'. Baadhi ya viongozi wenye ushawishi katika chama tawala cha Labor kama Peter Garrett na Ed Husic, wanatoa wito wa makubaliano ya kupata manowari zinazotumia nyuklia kutoka Marekani yachunguzwe upya.
Mvutano wa kidiplomasia umeibuka kati ya Afrika Kusini na Ghana kufuatia madai kwamba raia wa Ghana aliuawa wakati wa maandamano dhidi ya wahamiaji, madai ambayo maafisa wa Afrika Kusini wameyakanusha.
Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.






