Australia itatumia jumla ya dola bilioni 1.2 kutengeneza mamia ya magari ya kijeshi aina ya Bushmaster, na kuboresha magari yanayo lindwa aina ya Hawkei. Dola milioni 750 zimetengwa kutengeneza karibu magari 300 aina ya Bushmaster, ikiwa ni pamoja na magari yaliyo agizwa na serikali ya Uholanzi.
Polisi wanasema uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha moto ambao umesababisha vifo vya watoto wawili katika maeneo ya magharibi mwa Sydney. Haijulikani ambako wawili hao wako baada ya wengine watano wanaoishi katika nyumba hiyo, kufanikiwa kutoroka moto huo katika Mlima Bowen, ambao uko katika eneo la vilima vya Blue Mountain, baada ya saa nane usiku wa kuamkia.
Waasi wanaotaka kujitenga nchini Mali wa Touareg wakishirikiana na wapiganaji wa makundi ya itikadi kali wamefanikiwa kuchukua udhibiti wa mji muhimu wa kaskazini mwa Mali wa Kidal baada ya mashambulizi makali. Mamluki wa Urusi waliokuwa wakilisaidia jeshi la Mali wamethibitisha hivi leo kujiondoa katika mji wa Kidal na kwamba hatua hiyo imechukuliwa baada ya mashauriano na utawala wa Bamako, lakini wakasisitiza kuwa hali bado ni tete nchini humo.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.





