Wakati huo huo pia serikali inajaribu kukarabati, sehemu ya sera zake muhimu kama nishati. Ila mivutano ya wiki iliyopita imeingia katika wiki ya kwanza ya serikali mpya.
Katika taarifa zingine, Scott Morrison ameondoka nchini, akielekea Indonesia kwa ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama waziri mkuu.
Anatarajia kurejea nchini akiwa na makubaliano ya biashara huru yaliyoahidiwa kwa muda mrefu, pamoja na fursa yakuwasilisha ajenda hiyo bunge litakapofanya kikao tena baada ya wiki moja.





