Elewa haki za ardhi zawa Aboriginal nchini Australia

WAVE HILL WALK OFF 50TH ANNIVERSARY

Several thousand marchers celebrate the 50th anniversary Wave Hill Walk-off in Kalkarindji on Friday August 19, 2016. On August 22 1966 Vincent Lingiari led several hundred Gurindji people off Wave Hill Station in a protest to gain fair wages, which morphed into the battle for land rights, which took nine years to eventuate. Credit: AAP Image/Neda Vanovac

Unaweza sikia wito huu katika maandamano, “tuna taka nini? Haki za ardhi!” ila wito huo una maana gani? Ardhi iko katika kiini cha utambulisho, utamaduni na ustawi wa wa Aboriginal na watu kutoka Visiwa vya Torres Strait. Inajulikana kama “nchi” na inajumuisha ardhi, njia za maji, anga na kila kitu kilicho hai. Katika makala haya ya Australia ya Fafanuliwa, tuta chunguza haki za ardhi zawa Australia wa asili, wanacho husisha, ardhi gani ina funikwa, nani anaweza fanya madai na madhara kwa jamii za Mataifa ya Kwanza.


Key Points
  • Land rights return certain areas of Crown land — not private property — to Aboriginal and Torres Strait Islander communities for cultural, social, and economic benefit.
  • Land rights, native title, and treaty are different legal and political processes, but all aim to recognise First Nations peoples’ connection to Country and support self-determination.
  • The movement began with events like the 1966 Wave Hill Walk-Off, leading to landmark laws such as the Aboriginal Land Rights (Northern Territory) Act 1976, with progress still ongoing today.

Haki za ardhi zawa Aboriginal nchini Australia ni gani?

Kwa miaka mingi, uhusiano wa wa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait kwa ardhi yao haiku tambuliwa. Sheria kuhusu haki za Ardhi zili undwa kuwapa udhibiti kisheria kuhusu ardhi zao zakitamaduni.

Kabla ya ukoloni, wa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait, wali hudumia ardhi kwa makumi yama elfu ya miaka.

Ila, ukoloni ulichukua ardhi hiyo bila makubaliano yoyote, kulingana na wazo potofu la terra nullius maana yake Ikiwa ni “ardhi isiyo milikiwa na mtu yeyote.”
Gough Whitlam, Wave Hill Walk Off, Vincent Lingiari
Prime Minister Gough Whitlam symbolically returning land to the Gurindji people on 16 August 1975, an act famously represented by Whitlam pouring sand into Vincent Lingiari's hand. Source: AAP

Haki za ardhi zawa Aboriginal zili anzaje?

Harakati zakisasa za haki za ardhi zili anza katika mwaka wa 1966 kupitia maandamano ya Wave Hill Walk-Off — maandamano hayo yali ongozwa na wafugaji wa Gurindji stockmen pamoja na familia zao katika Wilaya ya Kaskazini.

Maandamano hayo yalimulika mazingira mabaya yakazi, pamoja na madai yakurejeshwa kwa ardhi zakitamaduni.

Katika mwaka wa 1967, kura ya maoni yakitaifa ili ipa Serikali ya Australia mamlaka yakutunga sheria kwa wa Aboriginal na watu kutoka Visiwa vya Torres Strait. Hatua hii ilifungua njia ya sheria ya 1976 ya Haki zawa Aboriginal (Wilaya ya Kaskazini) hii ilikuwa sheria ya kwanza kutambua madai ya ardhi ya jadi.

Baadhi ya majimbo na wilaya zina sheria zao binafsi za haki za ardhi, ila Australia bado haijawa na sheria moja ya kitaifa kuhusu haki za ardhi.

Haki za ardhi zawa Aboriginal zina funika nini?

Haki za ardhi zinatumika tu kwa ardhi inayo milikiwa na serikali inayo julikana pia kama, ardhi ya Taji — si mali binafsi. Ardhi inayo rudishwa, haiwezi uzwa au kuwekewa rehani. Badala yake, huhifadhiwa ili Jamii za Mataifa ya Kwanza zi ilinde nakufanya maamuzi kuihusu.

Baraza za Ardhi zili undwa kuwakilisha wa Aboriginal na watu kutoka Visiwa vya Torres Strait, na kuwasaidia kusimamia ardhi ambayo imerejeshwa. Baraza hizi husaidia jamii kutumia ardhi kwa sababu zakitamaduni, kijamii, mazingira na kiuchumi.

Tofatui ni gani kati ya haki za ardhi zawa Aboriginal, hati miliki ya asili na mkataba?

Ingawa mara nyingi hujadiliwa pamoja, maneno haya yana maanisha vitu tofauti:
  • Haki za Ardhi: Sheria zinazo tungwa na serikali zinazo rejesha baadhi ya ardhi ya serikali kwa watu waki Aboriginal na watu kutoka Visiwa vya Torres Strait, kawaida husimamiwa na baraza za ardhi. 
  • Hati miliki ya Asili: Kutambuliwa kisheria kuwa baadhi ya watu wa Mataifa ya Kwanza, bado wana haki kwa ardhi zao na maji chini ya sheria zao za jadi na mila. 
  • Mkataba: Makubaliano rasmi kati ya serikali na watu wa Mataifa ya Kwanza. Nchi kama New Zealand na Canada zina mikataba, ila Australia bado haijawa na mkataba wa kitaifa.
Pamoja, mbinu hizi zina lengo lakutoa haki, utambulisho na kujiamulia kwa watu wa Mataifa ya Kwanza.
wave hill sign.png
The Wave Hill walk-off, led by Vincent Lingiari, was a pivotal moment in Australian Aboriginal land rights history. In 1966, Gurindji stockmen, domestic workers, and their families walked off Wave Hill Station in protest against poor working conditions and a lack of land rights. Credit: National Museum Australia

Kwa nini haki za ardhi zawa Aboriginal ni muhimu leo?

Kurejesha ardhi husaidia jamii kuungana tena na lugha yao, utamaduni na Nchi. In saidia pia kwa swala la makaazi, afya, elimu na uhuru wa kiuchumi.

Dr Virginia Marshall, ni mwanamke wa ukoo wa Wiradjuri Nyemba, yeye pia ni mtaalam wa haki ya maji. Ame elezea umuhimu wa uhusiano ambao watu wa Mataifa ya Kwanza wanazo kwa ardhi na maji.

“Maji huzungumza nasi, au miti huzungumza nasi ila, silazima tuchukue itikadi ya mazingira ya Wazungu na mazungumzo, ambayo haya endani na uelewa wetu na sheria zetu na uelewa wetu hadithi zetu za uumbaji.”

Haki za ardhi hazi husu kuchukua nyumba au pango la mtu. Zina lenga kurejesha sehemu maalum za ardhi za Serikali, ambako kuna muunganisho waki historia au wakitamaduni.

Mfano wa ndani: Darkinjung Land Council

Shirika la Darkinjung Local Aboriginal Land Council, lililo undwa chini ya sheria ya Haki ya Ardhi yawa Aboriginal ya New South Wales, lina onesha uwezekano wa haki za ardhi katika matendo.

Uncle Barry Duncan, ni mwanaume kutoka ukoo wa Gomeroi, yeye pia ni mmoja wa waanzilishi wa shirika la Darkinjung Land Council, anakumbuka jinsi shirika hilo lili anza katika mwaka wa 1983 ndani ya pango la babake:

“Ili leta jamii hii pamoja. Ilikuwa mbinu yaku hakikisha ardhi ina wekezwa katika umiliki wawa Aboriginal”

Katika miaka iliyopita shirika la Darkinjung lime saidia kujenga fursa zaki uchumi na kuimarisha ufanyaji wa maamuzi ya jumuiya.

Uncle Barry anatafakari: “Sasa watu wanajua… tulikuwa na busara sana kwa swala la umiliki wa ardhi.”
MA25133794-Vincent-Lingiari-1200w.jpg
Vincent Lingiari beside a plaque marking the handing over of the lease in Wattie Creek, 1975. Credit: National Museum Australia

Changamoto za usoni ni zipi kwa haki ya ardhi yawa Aboriginal?

Mchakato wa haki za ardhi unaweza kuwa mgumu na wenye kasi ndogo. Ni kiasi kidogo tu cha ardhi kinapatikana kwa ajili yakurejeshwa, na baadhi ya madai yanakabiliwa kwa changamoto zakisheria au vizuizi vya kisiasa.

Licha ya changamoto hizi, haki za ardhi zina endelea kuwa sehemu muhimu ya njia ya Australia kuelekea kwa upatanisho, haki na kutambuliwa kwa kujitawala kwa Mataifa ya Kwanza.

Kwa nini haki za ardhi zawatu wa Asili ni muhimu kwa wa Australia wote?

Kwa watu ambao ni wageni nchini Australia, kujifunza kuhusu haki za ardhi ni mbinu yaku unganishwa na historia ya kina ya nchi. Hai husu kupoteza ardhi, inahusu kutambua nakurejesha mahusiano ya moja ya watu wakongwe duniani walio hai na ardhi.

Mahusiano haya yame dumu kwa zaidi ya miaka elfu 60,000 — na yana endelea hadi leo.
Jisajili au fuata makala yaliyo rekodiwa ya Australia ya fafanuliwa, kwa habari muhimu zaidi na vidokezo kuhusu kuanza maisha yako mapya nchini Australia.

Una swali lolote au wazo la mada? Tutumie barua pepe kwa: australiaexplained@sbs.com.au 

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service