Key Points
- A treaty is a formal agreement between governments and Aboriginal and Torres Strait Islander peoples
 - Many First Nations people see treaty as a step toward justice, respect, and better relationships in the future.
 - A national treaty would create a single, country-wide agreement for recognising Aboriginal and Torres Strait Islander rights across Australia.
 
- Kuna tofauti gani kati ya haki za ardhi ya Watu wa asili, Umiliki wa asili ya ardhi na mkataba?
 - Mkataba una maana gani?
 - Mkataba huu una umuhimu gani?
 - mkataba huu una nini?
 - Matarajio ya mkataba huu ni gani?
 

Protesters march from Parliament House to Flinders Street Station during the Treaty Before Voice Invasion Day Protest on January 26, 2023, in Melbourne, Australia. (Photo by Alexi J. Rosenfeld/Getty Images) Credit: Alexi J. Rosenfeld/Getty Images
Mkataba una maana gani Australia?
Mkataba ni makubaliano ya sheria yanayojadiliwa kati ya pande tofauti kwa mfano kati ya Waaboriginal na Torres Strait Islanders na serikali ya Australia.
Waingereza walipowasili Australia walitangaza ardhi kuwa ‘terra nullius’ kumaanisha ardhi isiyomilikiwa na yeyote. Hawakuona haja ya kuzungumza na mataifa ya waaboriginals na kwa hivyo wenyeji wa Australia wanasema kwamba hii ni biashara ambayo haijakamilika.
Mikataba hujengwa juu ya utambuzi wa enzi kuu na inaeza chukua mfumo tofauti tofauti huku ikishughulikia maswala anuwai
Australia, hata hivyo, haijawai kuwa na mkataba wa kimataifa unaowatambua watu wake wa kwanza ikilinganishwa na Marekani, Canada na pia New Zealand.
Kulingana na wenyeji, mkataba unamaanisha kutambua kilichotendeka hapo awali, kulinda haki na kuhakikisha kwamba Waaboriginal na watu wa visiwa vya Torres strait  wana sauti kwa maamuzi yanayowaathiri.
Mtalamu wa sheria Daktari Harry Hobbs anaeleza.
“mikataba ingejadiliwa kati ya jamii za Waaboriginals na Torrest strait islanders katika upande mmoja na serikali za majimbo na shirikisho. Hii ni kwa sababu katiba ya Australia inagawanya mamlaka kati ya bunge la shirikisho na bunge la majimbo.Dr. Harry Hobbs
Kuna mamia ya asili ya waaboriginals nchini Australia, kila moja ikiwa na lugha au kutoka maeneo tofauti, kwa hivyo mazungumzo yanaweza kuwa tatizo. Pia kuna mitazamo mbalimbali kuhusiana na kile kinachopaswa kupewa kipawa umbele.

(from left to right) Former Queensland Truth-Telling and Healing Inquiry chairperson Joshua Creamer, NSW Treaty Commissioner Naomi Moran and co-chair of the First Peoples' Assembly of Victoria Ngarra Murray. Credit: NITV / The Point
Mkataba huu una maana gani haswa?
Watu wengi wa jadi na pia kutoka visiwa vya Torres Strait wanaamini kwamba mkataba huu utaleta haki na heshima.
Kiongozi wa mkataba kutoka ukoo wa Gunditjmara Reuben Berg anatueleza umuhimu wake. 
nadhani mkataba ni muhimu sana, ni kuhusu kuweka upya uhusiano kati ya watu wa kwanza na serikali , iwapo kwenye ngazi ya jimbo au ngazi ya jumuiya ya madolaReuben Berg
Wafuasi wa mkataba wanasema kwamba italeta tofauti ya kweli kwa njia nyingi na wanaamini kwamba itawatambua waaboriginals na watu wa visiwa vya Torres strait kama watu wa kwanza wa Australia. Mkataba huu pia utafungua nafasi ya kuzungumzia historia ya nchii hii na ukoloni kwa uwazi.
Mkataba huu pia unatarajiwa kujenga uhusiano mwema kati ya serikali na jamii katika maeneo muhimu kama maji, ardhi, afya, elimu, makazi, ajira na maendeleo ya kiuchumi.
Watu wengi wa mataifa ya kwanza wanasema kwamba mkataba huu ni njia ya kulinda na kuimarisha lugha, tamaduni na maeneo takatifu ili kuhifadhi mila hizi kwa vizazi vijavyo.
Wakili kutoka ukoo ya Wirdi Tony Mcavoy anaeleza. 
Tunapoweza kudhibitisha Maisha yetu wenyewe, kufanya maamuzi sisi wenyewe na , tukijitolea huduma, tunakuwa wenye afya njema na nguvu zaidi, ustawi wa kiroho na wa kitamaduni. Ukikubali kwamba huo ni mojawapo ya matokeo ya mkataba huo, basi hiyo ni Habari njema kwa nchi nzima"Tony Mcavoy
Seneta Lidia Thorpe kutoka koo za Gunnai, Gunditjmara na Djab Wurrung, amekuwa mtetezi mashuhuri wa mkataba na anaamini kwamba jamii za maeneo ya wenyeji zinapaswa kuongoza mchakato huo.
Tunahitaji koo na mataifa kuwakilishwa katika ngazi ya serikali za mitaa. Ni jamii hizo ndizo zinaweza kuleta mabadiliko ya kweli.Lidia Thorpe

Independent Senator Lidia Thorpe during Question Time in the Senate chamber at Parliament House in Canberra. Source: AAP / MICK TSIKAS/AAPIMAGE
Hivyo basi, Nini kinaendelea Australia kuhusiana na mkataba?
Huku Victoria, mchakato wa mkataba unaendelea na makubaliano ya jimbo yanatarajiwa kufika mwaka 2025. Kupitia kundi lililochaguliwa linaloitwa Bunge La watu wa kwanza Victoria ama (First Peoples’ Assembly of Victoria) Waarboriginals watakuwa na sauti ya kudumu katika kuunda sheria na sera zinazohusu maswala yao.
Kwigineko, huko Queensland, New South Wales, South Australia, na Northern territory, maendeleo yako katika hatua tofauti. Baadhi ya serikali zinafanya mashauriano ya kijamii huku wengine wakipanga hatua zinazofuata.
Mkataba wa kitaifa utatengeneza makubaliano nchini Australia, huku mikataba ya majimbo na maeneo ikilenga vipaumbele vya ndani na mahitaji ya kila jamii.
Watetezi wengi wa watu wa asili wanaamini kwamba Australia inahitaji mikataba ya kitaifa na ya majimbo ili kuleta mabadiliko ya kweli na ya kudumu. Na kwa sababu kila jamii ina historia na mahitaji tofauti, kila mkataba utakuwa na sura tofauti.
Zaidi ya maana yake ya kisheria, mkataba pia unahusu uhusiano; jinsi Waaustralia wenye asili na wasio wa asili wanaishi na kufanya kazi Pamoja. Kwa wengi, mkataba huu ni hatua kuelekeza nchi yenye usawa na umoja zaidi, amabyo kila hadithi na jamii ina nafasi yake.
Kipindi hiki kina vipande vya sauti vilivyotolewa kwenye kipindi cha televisheni Living black-the case for a treaty ambayo ilionyeshwa kwa mara ya kwanza mwezi Julai mwaka 2025, na unaweza kutazama kipindi kizima kwenye sbs on demand.
Stream free On Demand
The Case For A Treaty
episode  •   Living Black • News And Current Affairs • 34m 
episode  •   Living Black • News And Current Affairs • 34m 
Jisajili au fuatilia Australia Explained kwa maelezo na ushauri zaidi kuhusu jinsi ya kuanza Maisha mpya nchini Australia na ikiwa una maswali au mada ungependa tuzungumzie tutumie barua pepe kwa australiaexplained.sbs.com.au.





