Hatakama katiba haitoi dhamana ya uhuru wa vyombo vya habari, Australia ni miongoni mwa nchi 29 katika Orodha ya nchi zenye uhuru wa vyombo vya habari.
Kwa hiyo, nafasi ya vyombo vya habari katika demokrasia ni gani? Vyombo vya habari binafsi na vinavyo wekezwa na umma vina tofauti gani nchini Australia?
Australia ina vyombo vya habari kadhaa, vinavyo jumuisha vyombo vya habari ambavyo vinamilikiwa na watu binafsi, pamoja na mitandao inayo fadhiliwa na umma.
Umma hufadhili pia vyombo viwili vya habari vya umma kupitia mapato ya kodi. Mashirika hayo mawili ya habari ya yanayo fadhiliwa na umma ni: Australian Broadcasting Corporation (ABC) na Special Broadcasting Service (SBS).
Vyombo vya habari vinavyo milikiwa na watu binafsi, huzalisha maudhui kwa ajili faida na ukadiriaji. Huwa vina toa majibu kwa wafadhili wao wakibiashara pamoja na maslahi yao. Kinyume chake, vyombo vya habari vya umma, huwajibika kwa umma unao vifadhili.