Hali hiyo ina ashiria umuhimu wakuakisi jamii wanazo wakilisha.
Mbunge huru mpya Dai Le alizungumza katika runinga ya jamii yawavietnam, kwa ajili yakuzungumza moja kwa moja na watu ambao walisaidia kumpa ushindi katika eneo bunge la Fowler ambalo liko katika eneo la Kusini Mashariki mwa Sydney.Ni eneo bunge lenye watu wengi wa asili ya Vietnam, na liliwahi kuwa ngome ya chama cha Labor kabla ya Bi Le kumshinda mgombea wa chama cha Labor Kristina Keneally.
Timu ya watu wenye asili mbali mbali, sura mpya zenye lengo lakubadilisha bunge la taifa.