Wakenya wanao ishi mjini Sydney, NSW walijumuika katika bustani ya Australia Botanic Garden kwa maadhimisho ya siku ya Mashujaa.
Wanajumuiya hao walishiriki katika matukio mbali mbali, na baadhi yao walichangia maoni yao na SBS Swahili kuhusu umuhimu wa maadhimisho hayo nchini Australia.