Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametangaza maombolezo ya kitaifa baada ya kufariki rais wa pili wa nchi hiyo, Daniel Arap Moi.
"Marehemu Moi aliongoza Kenya kwa utaratibu hadi ikarejelea mfumo wa vyama vingi vya kisiasa na pia kupitia changamoto nyingi hadi pale alipopokeza mamlaka kwa mrithi wake kwa njia ya amani mnamo mwaka wa 2002," alisema Kenyatta.
Moi aliongoza Kenya kuanzia mwaka 1978 hadi 2002, utawala wake chini ya mfumo wa chama kimoja ukigubikwa na madai ya mienendo ya kiimla, uvunjifu wa haki za binadamu na ubadhirifu.
Share





