Viongozi wakisiasa nakidini, wame adhimisha siku ya ijumaa ya pasaka, kwaku tathmini jinsi mwaka wakutengwa nakujitenga, umesaidia kuimarisha moyo wataifa, pamoja nakumulika uhaba wa usawa.
Umekuwa mwaka wenye changamoto kwa waumini ila, kuregezwa kwa vizuizi katika sehemu za ibada katika sehemu nyingi nchini, kume leta mabadiliko kwa wakristo. Baadhi walitumia fursa hiyo kuwa enzi wanao mulika ukosefu wa usawa ndani ya jamii. Askofu Mkuu wa kanisa laki Anglican Geoffrey Smith, alizungumzia giza la ubaguzi wa rangi pamoja na unyanyasaji wa nyumbani.
Wakati kanisa la Uniting, lili wahamasisha wanawake, waendelee kuzungumza, dhidi ya mashaka na jamii iliyo puuza sauti zao.