Watch FIFA World Cup 2026™

LIVE, FREE and EXCLUSIVE

SBS Examines:Nini inaweza fanywa kusimamisha kupandisha bei ya mafuta kwa njia ya unyonyaji?

fuel price gouging Landscape.00_15_57_05.Still004.jpg

As the fuel crisis continues, SBS Examines asked experts how Australians can be prepared for future fuel price shocks. Source: SBS / Dennis Fang

Bei za mafuta zimepanda, na wasiwasi pamoja na malalamiko kuhusu madai ya kupandisha bei kwa njia ya unyonyaji nao pia ume ongezeka. Je, wauzaji wa rejareja wanafaidika kupitia mgogoro huu?


Published

By Lera Shvets, Dennis Fang

Presented by Gode Migerano

Source: SBS




Share this with family and friends


Bei za mafuta zimepanda, na wasiwasi pamoja na malalamiko kuhusu madai ya kupandisha bei kwa njia ya unyonyaji nao pia ume ongezeka. Je, wauzaji wa rejareja wanafaidika kupitia mgogoro huu?


Tume ya Ushindani na Watumiaji ya Australia (ACCC) imesema wanachunguza wasambazaji wa maeneo ya kanda na vijiji vya Australia, katika hatua yakujibu malalamiko ya ada za ziada za mafuta za zaidi ya asilimia 70.

Ada za ziada za mafuta zimeripotiwa pia mijini kama ushuru katika migahawa, hotelini,na katika makampuni ya usafiri.

Matt Grudnoff, ni Mchumi Mkuu katika Taasisi ya Australia, ame ambia SBS Examines ni kinyume cha sheria nchini Australia kuwapotosha wateja- kwa mfano, kwa kutoa madai ya uongo kuwa ongezeko za bei zime sababishwa na ongezeko za gharama.

Hata hivyo, baadhi ya njia zingine za kupandisha bei kwa njia ya unyonyaji ni halali.

Watu wengi hawajui hivyo, ila si kinyume cha sheria kuongeza bei kwa njia ya unyonyaji.
Matt Grudnoff, senior economist, the Australia Institute

"Kama kampuni inaona kila mtu anazungumza kuhusu kupanda kwa bei na wanaamua kupandisha bei zao, hata kama gharama zao hazijapanda, hiyo ni halali kabisa." Bw Grudnoff alisema.

Professor David Byrne, Mwenyekiti wa Ritchie wa Utafiti wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Melbourne, alisema ushindani mzuri ni muhimu kwa ajili yaku kabiliana na kupandishwa kwa bei kwa njia ya unyonyaji.

Ila amesema pia kuwa, hii ni changamoto nchini Australia.

"Tuna makampuni machache yanayotusambazia. Na tunaona hilo katika mafuta. Tunaona hilo katika benki na maduka makubwa ya rejareja... makampuni haya yana nguvu za soko," alisema.

Unapokuwa na wachezaji wachache sokoni, uhaba wa ushindani unamaanisha utakuwa na bei za juu.
Professor David Byrne, the University of Melbourne

Katika makala haya ya SBS Examines, tunachunguza kupandishwa kwa bei kwa njia ya unyonyaji na kuuliza: Wa Australia wanawezaje jiandaa kwa mishtuko ya bei ya mafuta katika siku za usoni?

Ripoti za ziada kutoka SBS Nepali, SBS Russian na SBS Chinese.


Latest podcast episodes

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now