Amri zakubaki nyumbani zime ongezwa hadi baada ya mkutano wa dharura wa baraza lamawaziri wa jimbo la New South Wales. Aina ya kirusi cha Delta kime kuwa kikisambaa kwa kasi na, kusababisha kesi mpya 29, kesi 17 ambazo zilitangazwa Ijumaa 25 Juni 2021 zikijumuishwa.
Katika maendeleo mengine mwanaume mmoja na wanawake wawili wame kamatwa ndani ya chumba cha burudani katika Kijiji kimoja jimboni Kusini Australia, baada yakuvunja vizuizi vya mipaka, kwaku ingia kwa ndege jimboni humo kutoka kanda ya New South Wales.Zaidi ya idadi ya watu 1600 katika majimbo matatu wame amuriwa wajitenge baada ya mwanaume mmoja, kupatwa na coronavirus ndani ya mgodi ambao uko katika wilaya ya kaskazini.
Vipimo vya mfanyakazi wa mgodi huo vilirejesha matokeo chanya ya coronavirus Ijuaa, baada ya mwanaume huyo kuwasili wilayani tarehe 18 Juni. Kiongozi wa wilaya ya kaskazini Michael Gunner, amesema mwanaume huyo alipata virusi hivyo mjini Brisbane baada yakutakiwa kubaki ndani ya karantini hotelini kwa siku moja, kabla yakusafiri katika wilaya hiyo.
Serikali ya Wilaya ya Kaskazini ime weka maeneo pana ya kanda ya Darwin chini ya vizuizi, jimbo la Kusini Australia limefunga mipaka yake kwa majimbo mengine na maeneo ya mji wa Perth na wilaya ya Peel katika jimbo la Magharibi Australia, yame wekewa vizuizi ambavyo vitadumu kwa muda wa siku tatu. Jimbo la Magharibi Australia linakaza udhibiti wa mipaka yake kwa watu wanao wasili jimboni humo kutoka Victoria, Wilaya ya kaskazini, Queensland na ACT. Kila mtu anaye wasili kutoka wilaya na jimbo hizo lazima aingie katika karantini kwa muda wa siku 14 pamoja nakufanyiwa vipimo vya COVID-19.
Nalo jimbo la Kusini Australia limefunga mipaka yake na majimbo ya Queensland, Magharibi Australia, Wilaya ya Kaskazini na Australian Capital Territory. Ni wakaaji tu wa Kusini Austrlaia pamoja na watu ambao wana safari muhimu, ndiwo watakao ruhusiwa kuingia Kusini Australia kutoka majimbo hayo mengine. Wakaaji wa New South Wales wanaendelea kupigwa marufuku na wakaaji wote wa Victoria, kwa sasa lazima wafanyiwe vipimo vya virusi hivyo siku ya kwanza wanapo wasili Kusini Australia. Kwa msaada na hatua za afya ambazo zimewekwa, kujibu janga la COVID-19 katika lugha yako, tembelea tovuti hii: sbs.com.au/coronavirus