Tunapokabiliwa na matukio au itikadi zinazo enda kinyume na imani zetu binafsi, tunaweza hisi ambacho wataalam wanaita 'huzuni yakisiasa'. Baadhi wanasema inacheza nafasi katika ongezeko la mgawanyiko wa jamii yetu.
Je, maoni yako ya kisiasa yameathiri urafiki wako? Au labda unapata ugumu wa kujitambulisha na chama cha kisiasa ulichokuwa ukipigia kura?
Wataalamu wanaita hisia hii 'huzuni ya kisiasa', na wanasema inaweza sababisha mgawanyiko zaidi.
Profesa Larissa Hjorth kutoka Shule ya Vyombo vya Habari na Mawasiliano katika Chuo Kikuu cha RMIT ali ambia SBS Examines kwamba, huzuni ya kisiasa inajidhihirisha katika mgawanyiko wa vyombo vya habari, na wa jamii kwa ujumla. Jambo kuhusu huzuni ya kisiasa ni kwamba unapata aina hizo za vyumba vya mwangwi.
Jambo kuhusu huzuni yakisiasa ni kwamba, unapata aina hizo za vyumba vya mwangwi.Professor Larissa Hjorth, School of Media and Communication, RMIT University
""Mtu ambaye amejitambulisha na mrengo wa kushoto, mtu ambaye amejitambulisha na mrengo wa kulia, hawakutani kwa njia yoyote," alisema.
Taasisi ya Grattan hivi karibuni iligundua kuwa mgawanyiko wa jumla nchini Australia bado ni mdogo kuliko katika baadhi ya demokrasia zingine.
Ripoti yake mpya "Kwa watu: kulinda mustakabali wa demokrasia ya Australia" inaonyesha kwamba ni mtu mmoja tu kati ya Waaustralia 10 anayesema hawezi kuwa rafiki na mtu mwenye mitazamo tofauti ya kisiasa.
Hata hivyo, makubaliano ya kijamii ya nchi yako chini ya shinikizo.
Kate Griffiths, ni Naibu Mkurugenzi wa Programu ya Demokrasia katika Taasisi ya Grattan, alisema Waaustralia wanahisi kupungua kwa hisia ya kuwa sehemu ya jamii na fursa, na kuongezeka kwa hisia ya ukosefu wa haki.
Ni aina ya vitu vinavyoweza sababisha kutoshiriki au kutoridhika na mfumo wenyewe.Kate Griffiths, deputy director of the Democracy Program at Grattan Institute
Katika kipindi cha wiki hii, SBS Examines inachunguza huzuni ya kisiasa, na kusikia kutoka kwa baadhi ya Waustralia kuhusu uzoefu wao.
Makala haya yali tayarishwa kwa ushirikiano na SBS Mandarin.






